HTML na CSS

Lugha: Kiswahili
Utajifunza Nini?
    * Fahamu Coding ni nini na jinsi inavyofanya kazi
    * Kuwa na uwezo wa kuandika code kwa kutumia HTML na CSS
    * Kuw na Msingi mzuri wa kujiendeleza na Lugha zingine za kucode

Mahitaji
*  
Hii Course ni kwa ajili ya mtu ambae hana ujuzi kabisa
Ujuzi wa Basic English unahitajika

Maelezo

Anza safari yako ya Web Development na Design. Hii course itakuruhusu uendelee kwenye safari yako ya programming kwa njia rahisi na ya raha.
Programming imekuwa ni Ujuzi unaotafutwa na unaohitajika, sio kwa waajiri tu, ila kwa mtu yoyote anae taka ajitofautishe na wengine kwenye huu muda wa technolojia. Mwanzo wa safari yako unaweza ukajisikia kama vitu vinachanganya na kutisha. Unaweza ukajisiki kama mambo ni mengi ukiangalia lugha  zote ambazo unaweza ukajifunza. Hii course itahakikisha upate unachokitaka. Utajifunza vitu vya muhimu kwa mwendo mzuri utakao elewa, ili uanze ku code mapema iwezekenavyo!

HTML na CSS ni Lugha mbili za msingi ambazo kila programmer mpya inabidi afahamu. Kwenye course hii utajifunza ABC za zote mbili pamoja na kupata mazoezi ya kutosha ya kutengeneza website zinazo fanya kazi. Sasa unasubiri nini? Jiunge na Course leo uweze kuwa programmer!

Leave a comment